Na Mwandishi
Wetu, Nairobi
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano
ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya
ya Zanzibar Heroes, jana imetolewa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuzabwa
na Kenya
'Harambee Stars' mabao 2-0 kwenye mechi iliyochezwa jana mjini Nakuru.
Kwa matokeo hayo, Kenya
imeungana na timu za Ethiopia
na Jamhuri ya Sudani kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo
yanayosimamiwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA).
Mpira ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu
lakini, Kenya ilipata bao la
kwanza dakika ya tatu kupitia kwa Jockins Atudo kwa mkwaju wa penalti, baada
Mohamed Faki kumuangusha Francis Kahata katika eneo la hatari ndipo mwamuzi
Wish Yabrow toka Somalia
akaamuru ipigwe penalti.
Baada ya bao hilo, mpira uliendelea
kwa nguvu huku wachezaji wa Kenya
wakitumia nguvu nyingi ili kuwachanganya vijana wa Zanzibar .
Zanzibar Heroes ilifanya shambulizi kali dakika ya nane langoni
mwa Kenya na kupata faulo
iliyopigwa kwa shuti kali na Chile,
lililopanguliwa na kipa wa Kenya
na mpira kuokolewa na mabeki.
Dakika ya 18, Jacob Terry aliwapangua mabeki wa Zanzibar na kupiga shuti kali lililopanguliwa
kwa ustadi na kipa Abdallah Rashid.
Kipindi cha pili Harambee Stars iliingia kwa nguvu kutaka mabao
zaidi ambapo dakika ya 54, Alan Wanga aliipatia timu hiyo bao kwa mkwaju mkali
uliomshinda kipa Rashid.
Zanzibar Heroes ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Hamis Mcha 'Vialli'
na kumuingiza Ali Ali kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa upande wa ushambuliaji.
Hata
hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuisaidia Zanzibar
kwani Kenya
waliendelea kulichachafya lango la wapinzani wao, lakini kipa Rashid alikuwa
imara kupangua mashuti ya Mwanga na John Opio, waliokuwa wakiunganishwa vyema
na Kahata aliyekuwa akihaha uwanja mzima.
No comments:
Post a Comment